Na mwandishi wetu
WATU takribani bilioni saba duniani
hawamjui Mungu wa kweli kutokana na mafundisho ya kurithi ambayo yanatolewa na
viongozi wa dini mbalimbali kwa kutojua usahihi wa kile wanachowaaminisha
waamini wao.
Akizungunza jijini Dar es Salaam kuhusu hali ya umoja na uelewa wa watu kuhusu
imani ya dini, Nabii Joseph Buberwa idadi hiyo ya watu duniani hawaelewi kweli
Mungu wanayemwabudu na kumtumaini ni yupi.
Alisema viongozi wa dini zote
duniani wanawafundisha waamini wao kuacha maovu na kwamba watakwenda Mbinguni
baada ya maisha ya duniani kitua ambacho si kweli.
Nabii Buberwa alisema mbali ya
kwamba watu hawamjui Mungu wa kweli ambaye jina lake halisi ni Yehova, bado
kuna mambo makuu manne ambayo wameaminishwa kwa makosa na viongozi wao wa dini.
Aliyataja mambo hayo kuwa ni
kuaminishwa kwamba wanadamu waliokwenda kinyume na matwaka ya Mungu watachomwa
moto milele, maisha ya milele baada ya kifo ni Mbinguni, watu waliomcha Mungu
wote watakwenda Mbinguni na Shetani alikuwa mtawala wa dunia tangu mwaka wa
kwanza wa kuumbwa binadamu.
Alisema fundisho la kwamba watu wakifa kwa kumtumaini Mungu
wataishi milele Mbinguni si kweli na maisha ya milele yako duniani na kwamba
imeandikwa “Mshahara wa dhambi ni mauti” hivyo adhabu ya mtenda dhambi ni kifo
cha milele.
Nabii huyo alisema hawalaumu viongozi wa dini kwa kufundisha
mafundisho hayo ambayo ni potofu kwa kuwa hata wenye hawajui kwamba wanapotosha
na ufafanuzi wa maelezo hayo uko katika kitabu cha Sefania 3:8-9.
Kwa mujibu wa Nabii Buberwa, Mungu amempa mipango ya
kuwezesha vita vikomeshwe duniani ndani ya miaka saba ijayo, kuondoa uhalifu,
ufisadi, umasikini na njaa ndani ya miaka 14 tangu, Novemba 5, 2012.
Alisema watu wanaoamini kwamba baada ya kifo wakifufuliwa
watakwenda Mbinguni na waovu watachomwa milele wanaamini katika tumaini bandia
na hilo limefafanuliwa katika Ufunuo wa Yohana 5:9-10.
Hata hivyo alisema watu 144,000 tu ndio watakaokwenda
Mbinguni kutawala na Yesu Kristo na utawala huo utawahusu Watakatifu watakaokuwa
wako duniani baada ya maisha ya sasa kutoweka na waliokufa wakitekeleza amri za
Mungu watafufuliwa na kujumuika pamoja.
CHANZO
GAZETI LA JAMBO LEO

No comments:
Post a Comment