TAARIFA ya utafiti mpya inasema bado kuna watu milioni
774 duniani wasiojua kusoma na kuandika.
Shirika
la Umoja wa Mataifa linalohusika na Elimu, Sayansi na Utamaduni Unesco, lilitoa
ripoti wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kujua Kusoma na Kuandika Septemba nane
mwaka huu, iliyosema idadi kubwa ya watu hao mbumbumbu wanaishi katika mabara
ya Afrika na Asia.
Pia
takwimu za ripoti zinaonyesha kuwa robo tatu ya wale wasiojua kusoma na
kuandika ni wanawake,
na kwamba hali hiyo inaweza kuongezeka hata wakati wa kufikiwa tarehe ya mwisho ya malengo ya Maendeleo ya Milenia ambayo ni mwaka 2015.Katika ujumbe wake kuadhimisha siku hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova alisema kuwa dunia inapaswa kujikagua upya.
na kwamba hali hiyo inaweza kuongezeka hata wakati wa kufikiwa tarehe ya mwisho ya malengo ya Maendeleo ya Milenia ambayo ni mwaka 2015.Katika ujumbe wake kuadhimisha siku hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova alisema kuwa dunia inapaswa kujikagua upya.
Alisema
kuwa dunia ina wajibu wa kuboresha mifumo yake ya utoaji wa elimu, kwani
bila kufanya hivyo kuna uwezekano wa kurudi nyuma kimaendeleo. “ Tunapaswa
kumulika mifumo yetu ya utoaji elimu ili iende sambamba na mahitaji ya wakati”
anasema.
Wasiojua kusoma na kuandika Tanzania
Ripoti
hiyo ya Unesco imetolewa katika wakati ambapo kiwango cha kujua kusoma na
kuandika nchini kikitajwa kuporomoka.Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2002 idadi
ya Watanzania wasiojua kusoma na kundika ilifikia milioni 6.2.
Akizungumza
bungeni, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa alisema
kuwa idadi hiyo ni kwa watu wenye umri wa miaka 15 na kuendelea, sawa na
asilimia 31.
Aliongeza
kusema kuwa kuna uwezekanano idadi hiyo ikaongezeka kutokana na mazingira
yaliyopo sasa.
Alieleza
kuwa watu wasiojua kusoma na kuandika hawajamalizika, na kwamba Sensa ya Watu
na Makazi ya mwaka 2012 bado haikuwa imetoa mchanganuo wa watu
wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu.
“Ili
kuimarisha Elimu ya Watu Wazima, Serikali inatekeleza mambo mbalimbali, ikiwemo
kuboresha mpango wa awali wa Elimu ya Watu Wazima kupitia programu ya ‘Ndiyo
Naweza’ yenye lengo la kupunguza idadi ya wasiojua kusoma na kuandika nchini’’
anasema na kuongeza:
“Serikali
inatumia uzoefu uliopatikana katika utekelezaji wa Mpango wa Uwiano Kati ya
Elimu ya Watu Wazima na Jamii (MUKEJA), ambapo mpaka mwaka 2012 ulikuwa na
jumla ya wa
Wahitimu darasa la saba
Pamoja
na kuwepo kwa mikakati anayotaja Waziri Kawambwa, hali katika ngazi ya elimu ya
msingi haijawa nzuri. Tafiti zinaonyesha kuna idadi kubwa ya wanafunzi
wanaomaliza elimu ya msingi bila ya kujua kusoma na kuandika. Cha kushangaza
baadhi ya wanafunzi hao wamekuwa wakichaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari.
Kwa
mfano, Aprili mwaka jana, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ilibaini kuwepo
kwa wanafunzi wa sekondari 5200 waliokuwa hawajui kusoma na kuandika. Wanafunzi
hao walikuwa sehemu ya wahitimu wa darasa la saba mwaka 2011.
Awali
mwaka 2010, asasi isiyo ya kiraia ya Twaweza ilitoa ripoti ya utafiti
iliyobainisha kuwa kati ya wahitimu watano wa darasa la saba, mmoja hawezi
kusoma hadithi ya kiwango cha darasa la pili.
Utafiti
huo uliopewa jina la ‘Are Our Children Learning’ (Je, watoto wetu wanajifunza),
ulishirikisha sampuli ya watoto 42,033 kutoka kaya 22,800 nchi nzima.
Mikakati ya nchi
Tanzania
imekuwa ikitekeleza mipango mbalimbali yenye shabaha ya kuinua kiwango cha watu
kujua kusoma na kuandika. Miongoni mwa mipango hiyo ni ule ulianzishwa kwa mara
ya kwanza mwaka 1961ambao unatajwa kuwa ndiyo ulioweka misingi ya hali ya elimu
nchini. Idadi kubwa ya watu ilijitokeza na kujiunga katika taasisi za mafunzo
ya watu wazima.
Mpango
mwingine ulitekelezwa katika kipindi cha mwaka 1964 hadi 1969, na kuweka
mkazo wa kuboresha na kuinua elimu ya watu wazima, au maarufu ‘ngumbaru’ enzi
hizo.
Kupitia
mipango hiyo ya uendelezaji wa elimu wa watu wazima, inaelezwa kwamba hadi
kufikia miaka ya 1980, Tanzania ilikuwa ni moja ya nchi kadhaa duniani ambazo
watu wake wengi walikuwa wanajua kusoma na kuandika.
Kutokana
na hali hiyo, Umoja wa Mataifa uliitaja Tanzania kuwa ni moja ya nchi zilizoko
Kusini mwa Jangwa la Sahara ambayo imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuteleleza
mikakati ya kupunguza hali ya kutojua kusoma na kuandika.
Sio
kutajwa tu, Tanzania pia ilipewa tuzo maalumu kwa mafanikio hayo, ambayo watu
wengi wanayanasibisha na dhamira ya dhati aliyokuwa nayo Rais wa awamu ya
kwanza, Mwalimu Julius Nyerere.
Mafanikio
hayo yalichangiwa pia na uanzishwaji wa kampeni iliyoendeshwa katika maeneo ya
vijijini ambako ndiko kulikokuwa na idadi kubwa ya watu wasiojua kusoma na
kuandika .
nakisomo
907,771.’ Cha kushangaza inaelezwa kwamba kiwango cha kujua kusoma na kuandika
nchini, sasa kimeshuka kutoka asilimia 89.4 mwaka 1986 hadi ku¬fikia
asilimia 69 mwaka 2010.
Baadhi
ya wataalamu wa elimu wanasema kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka zaidi
katika kipindi cha miaka mitano ijayo kutokana na mwelekeo mpya wa sekta ya
elimu.
CHANZO MWANANCHI

No comments:
Post a Comment