Sunday, April 27, 2014

Mapapa wawili watangazwa watakatifu


 Na  Albano Midelo
Umati  mkubwa wa watu ulikusanyika mjini Vatican kushuhudia tukio la kihistoria ambapo viongozi wawili wa zamani wa Kanisa Katoliki, Papa John Paul II na Papa John XXIII wametangazwa watakatifu.
Ibada ya misa takatifu  iliyoendeshwa kwa pamoja kati ya Papa Francis na mtangulizi wake Papa Benedict XVI imeangaliwa na karibu mahujaji milioni moja
na wengine mamilioni ya watu kupitia matangazo ya  vyombo mbalimbali vya habari duniani kote.
Karibu ujumbe wa wageni 100 wamehudhuria sherehe hiyo, wakiwemo kutoka koo za kifalme na wakuu wa nchi na serikali.

 
Kumbukumbu za kanisa katoliki zinaonyesha kuwa hii ni mara ya kwanza kwa papa wawili kutangazwa kwa wakati mmoja kuwa watakatifu.

Kanisa katoliki duniani limesema bado linaendelea na mchakato wa kuwatangaza kuwa watakatifu hayati mwalimu Julius  Nyerere na Sr.Benadeta Mbawala wa Songea na kwamba mchakato ngazi ya Vatican unaendelea vizuri kwa kuzingatia hatua zote muhimu za mchakato. 
CHANZO MSAADA WA MTANDAO

No comments:

Post a Comment