![]() |
| Basi dogo la Imakulata ambalo abiria amesababisha kupinduka |
Na Albano Midelo
WATU wasiozidi 50 wamenusurika
kifo baada ya basi dogo linaloitwa Imakulata kupinduka katika eneo la Sinai nje kidogo ya mji wa
Songea mkoani Ruvuma kutokana na uzembe wa abiria .
Ajali hiyo ilisababisha
na mtu mmoja ambaye anadaiwa kuwa ni askari wa jeshi la kujenga Taifa JKT Mlale
Songea ambaye alikuwa ni mmoja wa abiria kuamua kuendesha basi hilo baada ya dereva
wa basi kutelemka na kumsaidia dereva
mwenzake ambaye basi lake lilikuwa limeharibika.
Dereva wa basi
lililopata ajali Bernad Bernad maarufu kwa jina la Kichefuchefu alisema yeye
baada ya kutelemka kwenda kumsaidia dereva mwenzake alishangaa kuona gari lake
linarudi nyuma likiendesha na mmoja wa abiria kisha kupinduka baada ya abiria huyo anayedaiwa kuwa ni mwanajeshi kushindwa
kulimudu kuendesha .
Bernad alisema kuwa
mabasi madogo matatu yalikodiwa na familia za
askari wa jeshi la kujenga Taifa Mlale ili kufika mjini Songea na kwamba
wakiwa katika eneo la Sinai ndipo basi moja lilikuwa na hitilafu ndipo mabasi
yote yalisimama ili kwenda kumsaidia mwenzao ili waweze kuendelea na safari ya
mjini Songea.
“ Baada ya kutelemka
nilishangaa kuona gari yangu inarudi nyuma kwa kasi kisha ikaanguka ikiwa na
abiria ambao walipata majeraha na kukimbizwa katika hospitali ya Peramiho,mtu
aliyesababisha ajali anayedaiwa kuwa ni askari wa JKT Mlale mara baada ya ajali
amekimbia msituni tulijaribu kumkimbiza tumeshindwa kumkamata’’,alisema Bernad.
Hata hivyo mwandishi
wakati anapita katika eneo la ajali hakuweza kukuta mtu yeyote aliyekuwepo
kwenye ajali hiyo zaidi ya dereva wa basi hilo,utingo na wapita njia ambao
walitoa lawama kwa askari huyo aliyeamua kuendesha gari wakati yeye alikuwa ni
abiria na kusababisha ajali kwa uzembe.
albano.midelo@gmail.com

No comments:
Post a Comment