Na Albano Midelo
Ukuaji
wa kiuchumi nchini Tanzania, taifa la tatu kwa kuzalisha dhahabu katika bara la
Afrika, ulifikia asilimia saba kwa mwaka tangu mwaka 2001.
Inadaiwa
katika kipindi cha miaka kumi wa utawala wa Rais wa awamu ya nne ukuaji wa
uchumi wa Tanzania uliendelea kusimama kwa asilimia saba huku nchi ikiwa na
rasilimali lukuki na ukuaji huo wa uchumi ukionekana zaidi kwenye makaratasi
huku wananchi kila kona ya nchi wakilia na umaskini na ufukara unaoendelea kwa
kasi.
Watanzania
wengi waliopo vijijini na mijini ni maskini zaidi wamekuwa na mabadiliko madogo
au hawajaona kabisa mabadiliko ya ubora wa maisha yao licha ya serikali kudai
inafanya vizuri kukuza uchumi wa Tanzania na kwamba mataifa makubwa eti yaliridhika
na kasi ya ukuaji wa Tanzania katika serikali ya awamu ya nne iliyoongozwa na
Rais mstaafu Jakaya Kikwete.
Kutokana
na umaskini unaendelea na kuwakabili wananchi wengi Tanzania ni miongoni mwa
nchi ambazo zimeshindwa kutimiza Malengo manane ya Maendeleo ya Milenia (MDGs)
ambayo mwisho wake ulikuwa ni mwaka 2015.
Wataalam
wa uchumi wa kimataifa wanasemaTanzania itahitaji miongo kadhaa ya ukuaji wa
kiuchumi kusaidia kuwaondoa watu wake katika ufukara na kutoa huduma muhimu za
msingi kama vile maji,huduma za afya,barabara na umeme.
Utafiti
umebaini kuwa ni watanzania wachache
wenye uwezo wa kupata huduma za msingi ambapo hivi sasa katika maeneo yote
mijini na vijijini wanakosa huduma muhimu kama maji na vituo vya kutolea huduma
za afya jambo ambalo ni hatari.
Wakati
taarifa za ukuaji wa uchumi kwenye
makaratasi zikionesha uchumi wa Tanzania unakua kwa asilimia saba kwa kipindi
cha miaka kumi iliyopita ya Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete, bado mamilioni
ya Watanzania wanaishi katika lindi la umaskini,baadhi yao wanapata mlo mmoja
kwa siku.
Nchi zinazotajwa kuwa tajiri
kama Malaysia,Taiwan na Singapore, zilikuwa kundi moja na Tanzania katika kundi la nchi maskini sana
duniani wakati tunapata uhuru mwaka 1961.Jambo la kusikitisha nchi hizo hazina
maliasili nyingi kama zilizopo Tanzania hali ambayo nchi zinazotuzunguka kama
Rwanda zinashangaa kwanini nchi yenye rasilimali nyingi kama Tanzania
inaendelea kuwa masikini badala ya kuwa nchi tajiri.
Bila shaka nchi imeshindwa kusonga mbele kwa miaka mingi kutokana na vitendo vya rushwa na ufisadi pamoja na sheria mbovu zinazosababisha nchi inashindwa kukusanya kodi ambazo serikali inastahili kuzipata.
Tunaamini hatua za dhati ambazo
zimeanza kuchukuliwa na uongozi wa serikali ya awamu ya tano zinaweza kusaidia
kuirudisha nchi katika njia yake hatimaye nchi inaweza kupaa kiuchumi na kuwa
miongoni mwa nchi zenye uchumi wa kati Duniani hata kabla ya mwaka 2025.
|
Tanzania imeeendelea kuhesabika kuwa miongoni mwa
nchi maskini kabisa duniani,huku pengo kubwa la watu masikini na matajiri
likiongezeka kwa kasi ya kutisha jambo ambalo linaleta chuki kwa wananchi
masikini ambao wanawaona watanzania wachache waliopewa dhamana kubwa
serikalini wakiwemo wabunge wakiishi katika maisha ya anasa.
Idadi kubwa ya watanzania hawana uhakika wa kupata
walau mlo mmoja wa siku,watu wanaishi katika nyumba zilizojengwa kwa tope na
kuezekwa kwa nyasi,watu hawana maji ya kunywa ,wanatumia vibatali na
mishumaa,watu wanalaa kwenye mkeka kwa ujumla maisha ya watanzania yapo enzi
za ujima.
Watumishi
wa ngazi ya chini serikalini wakiwemo walimu,polisi na wauguzi kutokana na
kulipwa mishahara midogo ambayo haikidhi hata wiki moja hivi sasa
wanakabiliwa na madeni makubwa kutokana na kukopa huku baadhi yao wakiwa
hawana mshahara kutokana na madeni hivyo wamekata tamaa ya kufanyakazi.
Wakulima licha ya kulima kwa shida kununua
pembejeo za kilimo kwa gharama kubwa bado serikali inawakopa mazao wanayolima
na kuongeza ugumu wa maisha.
Rais Magufuli amekuwa anasema Tanzania ni
nchi tajiri sana ina rasilimali lukuki na adimu,walioifikisha hapo Tanzania
ni mafisadi ambao wameiba fedha za serikali nyingine wamekwenda kuzificha nje
ya nchi,wamefuta azimio la Arusha ambalo lilikuwa linawabana kwa kuwa
mtumishi wa umma alikuwa haruhusiwi kujilimbikizia mali.
Hatua
ambazo zinachukuliwa na Rais Dk.Magufuli za kupambana na ufisadi wa
kuhakikisha kuwa vigogo wote serikalini bila kujali wadhifa wake ambao
wameiba mali za umma wafilisiwe na kuchukuliwa hatua za kisheria chini ya
mahakama ya mafisadi ambayo imeahidiwa kuundwa na serikali ya awamu ya tano
ili mali hizo zirudishwe serikalini na kutumika kwa manufaa ya watanzania
wote.
Tayari
ndani ya siku 100 za utawala wake Rais Magufuli amekusanya karibu shilingi
trilioni tatu,ameokoa shilingi bilioni saba ambazo zingetumika kwa safari za
nje za vigogo serikalini na anaendelea kupambana na wafanyabiashara wakwepa
kulipa kodi na watumishi wazembe.
Pia
mfumo wa upendelea serikalini ubadilishwe ambapo mianya yote ya kujinufaisha
vigogo serikalini ifutwe,sheria ya manunuzi serikalini ibadilishwe,posho za
kujipendelea kwa vigogo wakiwemo wabunge zifutwe badala yake mabilioni hayo
yatumika kwa manufaa ya watanzania wote na sio watu wachache wanafaidi keki
ya Taifa huku wengine wakipiga miayo kwa njaa.
Hayo
yakifanyika Tanzania yenye neema sawa kwa kila mtanzania inawezekana,kwa kuwa
sasa kila mmoja atanufaika na rasilimali za Taifa badala ya hali inayoendelea
sasa imejenga mafukara wengi huku watu wachache mabilionea wakitanua na
kufanya kila wanachotaka kutokana na nguvu ya fedha walionayo.
|

No comments:
Post a Comment