Na Albano Midelo
Awali ya yote
nampongeza Rais wa Jamuhuri ya Muuungano wa Tanzania katika serikali ya awamu
ya tano Dk.John Magufuli kwa kumteua
profesa Joyce Ndalichako kuwa waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
Nionavyo mimi Rais
Magufuli hajafanya makosa kumchagua profesa Ndalichako kutokana na uwezo mkubwa
ambao anao katika sekta ya elimu na hasa pale alipokuwa katibu mtendaji wa
Baraza la mitihani(NECTA) alifanyakazi
nzuri ambayo iliungwa mkono na wadau wengi wa elimu nchini.
Nionavyo mimi profesa
Ndalichako anaweza kuisimamia wizara ya elimu kwa ufanisi mkubwa na kupatia
ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili wizara hiyo kwa muda mrefu huku
wadau wengi wakiinyoshea wizara ya elimu kuchangia kushusha kiwango cha elimu
nchini.
Profesa Ndalichako
tangu alipoteuliwa na Rais Magufuli kuwa waziri wa elimu na hata kabla ya
kuteuliwa nafasi hiyo amekaririwa mara kadhaa katika vyombo vya habari
akisisitiza kubadili tafsiri ya ya elimu ya vyeti ambayo inafanyika hapa nchini
badala yake elimu ambayo inatakiwa sasa kuwekewa mkazo mkubwa ni elimu ya
vitendo na uelewa ambayo itajenga stadi muhimu kwa wahitimu wetu katika ngazi
mbalimbali za elimu nchini.
Nakubaliana na waziri
wa elimu kwamba wahitimu wengi katika vyuo mbalimbali ni wa vyeti kwa sababu mtu anaweza kupata alama za juu
katika cheti chake lakini katika hali halisi mhitimu huyo kichwani hana uelewa
kwa kile ambacho amesomea hivyo kushindwa kuitumia kwa vitendo elimu ambayo
ameipata iwe katika chuo kikuu au vyuo vingine.
Nionavyo mimi profesa
Ndalichako akipewa ushirikiano na wataalam wa elimu nchini anaweza kujenga ya
ubora wa elimu nchini kwa kuhakikisha kuwa changamoto zote zinazosababisha
kushuka kwa elimu kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Nionavyo mimi mfumo
mzima wa elimu ya Tanzania unatakiwa kubadilishwa kutoka elimu ya vyeti na kuwa
elimu ya vitendo kwa kuhakikisha wanafunzi wetu wanapatiwa ujuzi na stadi
muhimu za maisha ili kushindana na soko la ajira katika nchi nyingine ambazo
mfumo wao wa elimu ni wa vitendo na si vyeti.
Hata hivyo nionavyo
mimi waziri wa elimu anatakiwa pia kushughulikia changamoto mbalimbali
zinazowakabili walimu ambao ndiyo wadau muhimu katika sekta ya elimu kwa kuwa
wao wanawajibika moja kwa moja kutoa elimu kwa wanafunzi katika ngazi
mbalimbali.
Mfumo wa elimu ya
Tanzania kuanzia shule za awali hadi
elimu ya chuo kikuu unasababisha kupata wahitimu kila mwaka ambao hawana
maarifa na ujuzi ambao utawawezesha kujiajiri wenyewe.
Wahitimu wetu katika
vyuo vikuu walio wengi kutokana na mfumo mbovu wa elimu uliopo,umewafanya
waamini kuwa kupata cheti chenye alama ya juu ndiyo muhimu zaidi bila kujali
kupata ujuzi na maarifa ambayo yatakuwezesha kujiajiri mwenyewe na kuajiri
wengine.
Mfumo mbovu wa elimu
uliopo Tanzania ndiyo unasababisha watanzania kushindwa katika soko la ajira la
kimataifa kwa kuwa unaposhindana na wananchi wanaotoka katika nchi zenye mfumo
mzuri wa elimu ambao unazingatia maarifa na vitendo hauwezi kushindana nao .
Nionavyo mimi
watanzania wanatakiwa kujifunza katika nchi ambazo mfumo wao wa elimu ni imara
hauyumbishwi na wanasiasa.Kuna baadhi ya nchi wataalam wa elimu ndiyo
wameachiwa kusimamia elimu kulingana na sera na sheria katika nchi zao.
Nionavyo mimi elimu
ya Tanzania sio imara ukilinganisha na nchi nyingine ndiyo maana hadi sasa kwa
mfano ukiangalia hakuna kitabu cha somo moja ambacho kinaweza kutumika katika
nchi nzima kwa shule za msingi hali ambayo inasababisha kila shule kuamua kutumia kitabu chake wakati wanafunzi
wote wanafanya mtihani wa Taifa mmoja.
Maendeleo
ni vita

No comments:
Post a Comment