NA KWIRINUS MAPUNDA,SONGEA
Vikundi vya
wajasirimali kutoka mitaa 95 ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma vinatarajiwa
kuwezeshwa mikopo ya jumla ya shilingi
bilioni 4.95 sawa na kila mtaa kupata
shilingi milioni 50.
![]() |
| Abdul Mshaweji meya wa manispaa ya Songea akifungua mafunzo |
Afisa habari wa
manispaa ya Songea Albano Midelo alisema fedha hizo zinatokana na mpango wa
uwezeshaji wananchi milioni 50 kwa kila kijiji au mtaa ambazo zinatolewa na
Rais Magufuli kwa mkopo wa masharti nafuu.
Kulingana na afisa
habari huyo Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi tayari limetoa
mafunzo ya mpango wa uwezeshaji wananchi milioni 50 kila mtaa ambapo katika
manispaa ya Songea vikundi mbalimbali vilipata mafunzo hayo viwemo vyama akiba
vya kuweka na kukopa SACCOS na VICOBA.
Akizungumza wakati wa
ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo,Mstahiki meya wa manispaa ya Songea Abdul Hassan
Mshaweji aliviasa vikundi vyote ambavyo vitapata mkopo nafuu wa milioni 50
kuhakikisha kuwa kila mwanakikundi kulipa mkopo huo kwa wakati ili kila mmoja
anaweze kunufaika.
“kila mtaa katika
manispaa yetu utapata milioni 50 hivyo kwa mitaa yote 95 tunapata shilingi
bilioni 4.75,naomba kila mwananchi awe na tabia ya kuweka akiba,kukopa kwa
busara,kulipa kwa wakati na kila aliyekopa akumbuke kurudisha pesa hizo kwa
kuwa ni mkopo unatakiwa kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa’’,alisisitiza
Mshaweji.
![]() |
| Wakazi wa manispaa ya Songea wakifuatilia mafunzo |
Mstahiki Meya huyo
aliwaasa wote watakaopata mkopo huo kuhakikisha kuwa wanafanya matumizi yatakayowaletea maendeleo
kwa kuwa uzoefu unaonesha kuwa watanzania wengi hawana matumizi ya fedha
yaliyokusudiwa hivyo aliwaonya fedha hizo sio kwa ajili ya kufanya sherehe bali
ni kwa ajili ya maendeleo.
Mshaweji alisema
Tanzania inakwenda kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 ambapo kipato cha
kati ya mtanzania kwa siku kinatarajia kuwa shilingi 67,000 na kwamba uchumi wa
kati unakwenda sanjari na kuanzisha
viwanda vidogo na vya kati.
Akitoa mafunzo ya
mpango wa uwezeshaji wananchi milioni 50
za Rais Magufuli kwa kila mtaa na kijiji
kwa mamia ya vikundi vya ujasirimali katika ukumbi wa manispaa ya
Songea,mkurugenzi wa mifuko ya uwezeshaji nchini Edwin Chrisant alisema Baraza
la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi
litasimamia na kuhakikisha kuwa mkopo huo unatolewa bila ubaguzi wa aina
yoyote.
![]() |
| Edwin Chrisant mkurugenzi wa mfuko wa uwezeshaji akitoa mafunzo |
Chrisant aliwaasa
wananchi kuchukua mkopo huo kwa busara na kurejesha kwa utaratibu na
kuwakumbusha wale wote waliochukua mkopo wa mabilioni ya Rais mstaafu wa awamu
ya nne ambao hawajarejesha mikopo yao wanafahamika na wajiandae kutumbuliwa.
Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi
tayari limetoa mafunzo ya mpango wa uwezeshaji wananchi milioni 50 kwa kila
kijiji na mtaa katika Halmashauri tatu za mkoa wa Ruvuma ambazo ni Songea
vijijini,Mbinga na Songea manispaa.
Chimbuko la kutolewa
mkopo huo wa masharti nafuu katika vijiji na mitaa yote Tanzania linatokana na
ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2015 ibara ya 57 ambapo
CCM iliahidi kuwawezesha wananchi kiuchumi endapo kingefanikiwa kuingia
madarakani.
Uwezeshaji wananchi
ulioahidiwa katika ilani hiyo ni pamoja na Kutenga shilingi milioni 50 kwa kila kijiji au mtaa kama mfuko wa
Mzunguko (Revolving Fund) kwa ajili ya kuvikopesha vikundi vya wajasiriamali
kupitia SACCOS na VICOBA,Kusimamia uanzishwaji wa vikundi vya ushirika
kama SACCOS na VICOBA na Kuweka mfumo wa kuvitambua na kuvisajili na
Kuhakikisha upatikanaji wa mitaji yenye masharti nafuu bila urasimu wowote.
MWISHO



No comments:
Post a Comment