Mwanamke huyo
alipachikwa mimba kupitia njia ya kitaalamu ya IVF ambapo yai la mwanamke
hutolewa kutoka kwenye ovari, kutungishwa mbegu ya kiume na kisha kurejeshwa
kwenye mji wa mimba. Yai hilo linaweza kutolewa kwa mwanamke mwingine.
Njia hiyo hutumiwa
kuwawezesha wanawake tasa kupata watoto.
Daljinder Kaur
alijifungua mtoto wake baada ya kupokea matibabu kwa miaka miwili katika
hospitali iliyoko jimbo la Haryana.Matabibu walifanikiwa kumtungisha mimba
kupitia IVF mara yao ya tatu.Mumewe Kaur ana umri wa miaka 79.
Kisa hicho kimezua mjadala mkali kuhusu
kutumiwa kwa teknolojia hiyo ya IVF na umri ambao wanawake wanaweza kuruhusiwa
kuitumia kupata watoto.Dkt Kanad Nayar, katibu mkuu wa chama cha upachikaji mimba nchini India anasema sheria ya kuamua umri wa juu ambao mwanamke anaweza kuruhusiwa kutumia teknolojia hiyo itatungwa karibuni.
![]() |
| Mwanamke aliyejifungua mtoto akiwa na mumewe |
Sana umri huo utakuwa miaka karibu miaka 55.Daktari huyo anasema jambo la kuzingatiwa zaidi ni uwezo wa mwanamke kumlea mtoto hadi akomae
"Ukimzaa
mtoto lazima uweze kumlea mtoto kwa karibu miaka 20 hivi. Huwezi kujifungua
mtoto kisha uwaache watu wengine wakimlea,” amesema Dkt Nayar.
Ni mara ya pili
kwa mwanamke mkongwe kujifungua mtoto India. Awali, mwanamke wa miaka 70
alijaliwa mtoto nchini humo.
Lakini mwanamke
huyo alifariki miaka miwili baadaye na sasa mtoto huyo anatuzwa na jamaa zake
http://www.bbc.com/swahili/habari/2016/05/160511_72_woman_birth


No comments:
Post a Comment