Na Julius Konala
Taarifa ya mdhibiti
na mkaguzi mkuu wa Hesabu za serikali(CAG)
imetoa Hati Safi katika miradi yote mitatu ya Halmashauri ya manispaa ya
Songea mkoani Ruvuma.
![]() |
| Jenifer Omolo mkurugenzi wa manispaa ya Songea |
Ofisa habari wa
manispaa ya Songea Albano Midelo ameitaja miradi iliyopata Hati Safi katika
manispaa hiyo kuwa ni pamoja na mradi wa
maji(NWSDP),mradi wa afya Health Basket
Fund(HBF) na mradi wa kilimo na mifugo Agriculture Sector Development
project(ASDP).
ilipokea taarifa za miradi hiyo mitatu kutoka kwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali katika kipindi cha mwaka 2014/2015 ikionesha miradi yote mitatu imepata Hati Safi.
Hata hivyo amesema
hivi sasa menejimenti ya manispaa hiyo inaendelea na mchakato wa kujibu hoja
ambazo zimetolewa kwenye miradi hiyo kisha kupelekwa kwa CAG kwa ajili ya
kuhakikiwa,kufungwa na kufutwa kwa hoja zinazohusika ndani ya siku 21 kuanzia
Juni 8 mwaka huu.
Wakati huo huo
Halmashauri ya manispaa ya Songea imependekeza kufuta wadaiwa saba sugu
wanaodaiwa zaidi ya shilingi milioni
14.7 katika kipindi cha kuanzia mwaka 2011/2012 ambapo Halmashauri ya manispaa
hiyo ilipata Hoja za Ukaguzi ambazo zilitokana na kutokusanywa kwa fedha za mtu
binafsi na vikundi vya wanawake kutokana
na kukosa kumbukumbu na orodha ya vikundi.
Ofisa habari huyo wa
manispaa ya Songea anabainisha kuwa vikundi vya wanawake katika kipindi cha
mwaka 1997 hadi 2012 walikuwa wanadaiwa
zaidi ya shilingi milioni 10 na kwamba Hoja ya kudaiwa vikundi hivyo hadi leo
bado haijafungwa kutokana na wadaiwa kutoilipa manispaa.
“Ufuatiliaji uliofanyika unaonesha kuwa
wadaiwa wote hawajulikani walipo kwa kuwa vikundi,orodha yao haipo na aliyekuwa
mratibu wa kazi ya vikundi hivyo amefariki Dunia, kwa kuwa Hoja hiyo imeendelea
kuwepo hadi sasa mweka hazina mkuu wa
manispaa ya Songea amependekeza kufutwa kwa wadaiwa hawa’’,alisema.
Alisema mwaka
2011/2012 Halmashauri ya manispaa ya Songea ilipata Hoja za ukaguzi namba
2.2.10.2 ambayo ilitokana na kutokusanywa kwa fedha za pango za kituo cha
mabasi kwa wapangaji sita ambao wanadaiwa jumla ya shilingi milioni 4.6
kwa mwaka wa fedha wa 2007/2008 unaoishia Juni 30 mwaka huu na kwamba hoja
haijafungwa hadi sasa ambapo wadaiwa hawajulikani na wamefunga vibanda vyao.
Amewataja wadaiwa
sugu hao kuwa ni Nassoro Suleiman anadaiwa kuanzia Juni 2009 hadi Mei 2016
jumla ya shilingi 400,000,Kilimanjaro Express kuanzia Januari 2007 hadi Mei
2016 jumla ya shilingi milioni 1.65,Martin Massawe kuanzia Januari 2007 hadi
Mei 2016 jumla ya shilingi 600,000,Mr.Nyaruke kuanzia Januari 2007 hadi Mei
2016 shilingi milioni 1.8 na Esta Komba kuanzia Januari 2007 hadi Mei 2016
shilingi 150,000.
Kwa mujibu wa kifungu
cha local Authorities Financial Memorandum cha mwaka 2009,LAFM Order 44(3)
kinaeleza kufuta wadaiwa sugu na kifungu 104(2) cha local authorities Financial
Memorandum cha mwaka 2009 kimeweka umri wa zaidi ya miaka mitano kama kigezo
cha madai yasipolipwa kufutwa.
Mwisho.

No comments:
Post a Comment