NA
KWIRINUS MAPUNDA,SONGEA
Katibu mkuu wa wizara
ya habari,utamaduni,sanaa na michezo Profesa Elisante Ole Gabriel amewaasa
wanahabari nchini kutoa habari sahihi na
kwa usahihi wake ili kuepusha madhara ya upotoshaji wa habari.
Profesa Gabriel
ametoa wito huo mjini Songea katika
ziara yake ya kawaida ambapo amefanikiwa kufanya kikao na wadau
mbalimbali wa habari kutoka katika Halmashauri za Mbinga, Nyasa, amtumbo,Tunduru,Madaba,manispaa ya Songea na Songea vijijini.
Amesema habari
inaweza kuwa potofu lakini ikatolewa
vizuri na kwa usahihi na kwamba habari inaweza kuwa sahihi lakini ikashindwa
kutolewa vizuri na kwa usahihi hivyo jambo muhimu kwa mwandishi ni kutoa habari
sahihi na kwa usahihi wake
hali ambayo itasaidi kuelimisha jamii kutokana na
habari kuwa sahihi.
“Sekta ya habari
ikifanyika kwa weledi inaweza kuleta mabadiliko chanya kwa watanzania lakini
ikitolewa kwa kupotoshwa inaweza kuleta madhara makubwa hata kusababisha
kifo,nawaomba wadau wote wa habari fanyeni kazi kwa kufuata taratibu,kusimamia
sheria na kanuni zilizopo’’,alisema Profesa Gabriel.
Hata hivyo
amewakumbusha wadau wa habari kuacha urasimu katika kutoa habari sahihi kwa
wadau na kusisitiza kuwa jamii
itakukumbuka kutokana na mchango ambao uliutoa kabla ya kustaafu na wala sio
muonekano wako au elimu ulionayo.
Katika ziara
hiyo katika manispaa ya Songea katibu
mkuu ametembelea maeneo mbalimbali
ambayo yapo chini ya wizara yake yakiwemo Makumbusho ya Taifa ya Majimaji ya
Songea,kituo cha redio ya Taifa kanda ya kusini Songea pamoja na kituo cha
redio binafsi cha Jogoo Fm cha mjini Songea.
Katibu mkuu pia
amewakabidhi vifaa vya kisasa vya mawasiliano aina ya IPAD vilivyofadhiliwa na
shirika la Startimes, maafisa habari wanne kutoka katika mkoa wa Ruvuma akiwemo
afisa habari wa mkoa wa Ruvuma,afisa habari wa manispaa ya Songea,afisa habari
wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo na afisa habari wa Halmashauri ya wilaya
ya Tunduru.
Katika ziara hiyo ya
siku moja katibu mkuu pia amekutana na wadau katika sekta za michezo,sanaa na
utamaduni wakiwemo wenyeviti na makatibu
wa vyama vya michezo ngazi ya mkoa.
Katibu mkuu huyo
anafanya ziara ya kikazi katika mikoa ya ukanda wa kusini kwenye mikoa ya Iringa,Njombe,Ruvuma,Lindi na
Mtwara lengo likiwa ni kuipeleka wizara
ya habari, utamaduni, sanaa na michezo kwa wadau mikoani.
Mwisho.

No comments:
Post a Comment