Thursday, June 9, 2016

Yaliojiri mapokezi ya Mwenge wa Uhuru manispaa ya Songea

Mwenge wa uhuru katika manispaa ya Songea umefanikiwa kufungua miradi sita katika maeneo mbalimbali ya manispaa ya Songea ukiwemo mradi wa madawati 100 katika shule ya msingi Luhira,kupandamiti chanzo cha maji ya SOUWASA,kufungua stendi ya mabasi ya Songea mjini,uzinduzi wa nyumba ya mkurugenzi wa manispaa ya Songea,madarasa mawili katika shule ya sekondari Chabruma na mradi wa ng'ombe wa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI katika eneo la mwenge mshindo.
Mwenge wa uhuru katika manispaa ya Songea umeweza kufanya miradi hiyo yote kwa amani na usalama ambapo katika miradi hiyo yote mamia ya wakazi wa manispaa ya Songea walijitokeza kwa wingi ikiwa ni pamoja na kukesha hadi asubuhi,wakishangilia na kucheza hata baada ya mwenge kuondoka katika eneo la mkesha katika shule ya Kibulang'oma.
 Mwenge wa uhuru ulimaliza salama mbio zake katika manispaa ya Songea na Juni 9  mwaka huu ulikabidhiwa katika Halmashauri ya Mbinga.



Mwenyekiti wa ulinzi na usalama wilaya ya Songea ambaye ni mkuu wa wilaya ya Songea Benson Mpesya akiwa katika mapokezi ya mwenge wa uhuru hapa mwenge ulikuwa unaingia katika chanzo cha maji cha Luhira ambacho kinategemewa na Mamlaka ya maji safi na maji taka Songea SOUWASA ambapo kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2016 aliongoza kazi ya upandaji miti kwenye chanzo hicho muhimu katika manispaa ya Songea
Mwenge wa uhuru ukiwa mpakani mwa wilaya ya Namtumbo na Songea katika kijiji cha Shule ya Tanga
Katibu tawala wa wilaya ya Songea akisoma risala ya utii kwa Rais katika majumuisho ya mbio za mwenge kitaifa manispaa ya Songea kwenye viwanja vya kibulang'oma
Mradi wa madarsa mawili katika shule ya sekondari Chaburuma manispaa ya Songea ambayo yalifunguliwa na Mwenge
Mwenge wa uhuru ukiwa unaingia katika stendi ya mabasi ya mjini Songea kwa ajili ya uzunduzi wa stendi hiyo
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2016 akiwa ndani ya stendi  ya mabasi ya Songea baada ya kufanya uzinduzi
Viongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa wakiwa Songea TTC
Madawa ya kulevya ambayo yalikamatwa na polisi yakichomwa siku ya mbio za mwenge kitaifa 2016 shule ya msingi Mloweka
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa akiwa na mkuu wa wilaya ya Songea pamoja na mkurugenzi wa manispaa ya Songea katika chanzo cha maji cha SOUWASA ambako ilifanyika kazi ya upandaji miti kitaifa
Mbio za mwenge wa taifa zikiingia kufanya uzinduzi wa nyumba ya mkurugenzi wa manispaa ya Songea,nyumba hiyo inatarajia kugharimu zaidi ya shilingi milioni 200 ambapo hadi sasa zaidi ya milioni 80 zimetumika
Mbio za mwenge wa uhuru stendi ya mbasi Songea
Wanakwaya wa Songea TTC  wakitumbuiza siku ya mwenge
Vijana wadogo wakitumbuiza siku ya mapokezi ya mwenge wa uhuru kitaifa
Kiongozi wa mbio za  mwenge kitaifa akipanda mti katika chanzo cha Ruhila
Kikundi cha ngoma ya mganda katika kijiji cha Mwengemshindo wakitumbuiza siku ya mwenge
Mwenge wa uhuru ukiwa katika kijiji cha Mwengemshindo Songea mjini

Add caption

No comments:

Post a Comment