Kila mtumishi wa umma awajibike
Mkuu wa mkoa wa
Ruvuma Dk.Binilith Mahenge
amewaagiza watumishi wa umma mkoani humo
kuwajibika kwa wananchi na kuwaondolea kero mbalimbali zinazowakabili.
Dk.Mahenge alitoa agizo hilo wakati anazungumza na wakuu wa idara wa manispaa na Taasisi za umma kwenye kikao na viongozi wa wazee na wafanyabiashara kilichofanyika kwenye ukumbi wa manispaa ya Songea.
Ameagiza watumishi
wote wa umma kufanya jitihada za dhati za kuwaondolea kero wananchi katika
maeneo yao na kusisitiza kuwa watendaji wasiwe chanzo cha kero
katika maeneo
ambayo wanayaongoza.
“Nataka kuona matokeo
mazuri kwa kila kazi inayofanywa na mtumishi wa serikali,tabia ya kuorodhesha
kero,changamoto,na matatizo siyo suluhisho la utendaji kazi.Lugha za njoo
kesho,tupo kwenye mchakato sasa zifikie mwisho kwa watumishi wanaowahudumia
wananchi’’,alisisitiza.
Dk.Mahenge amewaagiza
viongozi wa Taasisi mbalimbali za umma
kufanyakazi kwa waledi wa taaluma zao ili kutoa huduma kwa wananchi katika
kiwango cha ubora unaohitajika.
Hata hivyo mkuu huyo
wa mkoa amewapongeza wananchi na wadau wote wa maendeleo kutokana na kuunga
mkono jitihada mbalimbali za serikali ya awamu ya tano ambazo zimesababisha
kufikia malengo ambayo yameanza kuonekana.
Kwa upande wake
mbunge wa Songea mjini Leonidas Gama amewaasa wakazi wa manispaa ya Songea
kumpa ushirikiano mkubwa mkuu wa mkoa mpya ambapo amesema mkoa umempata mkuu wa
mkoa mchapakazi ambaye anaweza kuupaisha mkoa huo kulingana na malengo ya
serikali ya awamu ya tano.
Gama amewaasa wakazi
wa manispaa ya Songea na watumishi wa umma sasa kila mmoja achape kazi badala
ya kujiingiza kwenye migogoro ya wanasiasa hivyo kuzorotesha maendeleo
endelevu.
Rais Dk.John Magufuli
amemteua Dk.Binilith Mahenge kuwa mkuu
mpya wa mkoa wa Ruvuma ambaye amechukua nafasi ya aliyekuwa mkuu wa mkoa huo
Said Mwambungu ambaye amehamishiwa ofisi ya waziri mkuu.
Mwisho.

No comments:
Post a Comment